Kufungua kifungo cha juu cha kanzu

Swali: Je, ni katika Sunnah kufungua kifungo cha juu cha kanzu?

Jibu: Hilo halidhuru. Ama kufungua kifungo kwa njia ya kwamba kifua kikabaki wazi, wanachuoni wamesema kuwa jambo hili linaenda kinyume na muruwa. Jengine pia ni mtu akaikunjua miguu yake mbele za watu. Hili pia linaenda kinyume na muruwa. Ama kufungua kifungua kifungo cha juu kwa sababu joto kali haina madhara.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 22/02/2019