Swali: Je, inajuzu kufunga siku aliyozaliwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hapana. Swawm haikuwekwa katika Shari´ah na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hatukuwekewa Shari´ah tufunge. Ndio, funga kila jumatatu, sio kwa sababu tu imeangukia tarehe 12 Rabiy´ al-Awwal. Funga jumatatu ya kila wiki ndio Sunnah. Ama kufunga jumatatu kwa sababu tu imekutana na 12 Rabiy´ al-Awwal unashereheka kwa sababu ni siku ya mazazi yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), haijuzu kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/7428
  • Imechapishwa: 06/11/2019