Swali: Nimesikia kuwa ni haramu kufunga jumamosi peke yake. Nitakuwa nimetenda dhambi nikifunga siku ya ´Aashuuraa´ ikiangukia siku ya jumamosi?

Jibu: Hapana. Hukukusudia kufunga siku ya jumamosi, umekusudia kufunga ´Aashuuraa´. ´Ashuuraa´ imewekwa katika Shari´ah kuifunga. Wala sio haramu kufunga siku ya jumamosi. Imechukizwa. Wanachuoni wanasema kuwa imechukizwa kufunga Rajab, ijumaa peke yake na jumamosi peke yake. Ima mtu aifunge pamoja na siku kabla yake au baada yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%204%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2017