Kufunga siku sita za Shawwaal ni Bid´ah?

Swali: Unasemaje juu ya yule mwenye kusema kwamba kufunga siku sita za Shawwaal ni Bid´ah na kwamba haya ni maoni ya Imaam Maalik? Akipewa dalili ya Hadiyth ya Abu Ayyuub:

“Atakayefunga Ramadhaan kisha akaifuatishia siku sita za Shawwaal basi ni kama ambaye amefunga mwaka mzima.”[1]

anasema kwamba katika cheni ya wapokezi wake kuna mtu ambaye ametiwa dosari.

Jibu: Maneno haya ni batili. Hadiyth ya Abu Ayyuub ni Swahiyh. Hadiyth hiyo ina zengine zenye kuisapoti na kutolea dalili maana yake.

[1] Muslim (1164), at-Tirmidhiy (759), Abu Daawuud (2433), Ibn Maajah (1716), Ahmad (05/417) na ad-Daarimiy (1754).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/390)
  • Imechapishwa: 08/06/2018