Swali: Kuna masiku kunafungwa swawm ya kujitolea katika mwezi wa Rajab. Je, masiku hayo yanakuwa siku za mwanzo, katikati au mwishoni?

Jibu: Hakukuthibiti Hadiyth maalum juu ya fadhila za swawm ya Rajab mbali na yale aliyopokea an-Nasaa´iy, Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah akaisahihisha kupitia Hadiyth ya Usaamah aliyesema: “Nilimuuliza: “Ee Mtume wa Allaah! Hatukukuona unafunga mwezi wowote kama unavyofanya Sha´baan.” Akasema: “Huo ni mwezi ambao watu wengi wanaghafilika kwao baina ya Rajab na Ramadhaan. Huyo ni mwezi ambao matendo yanapandishwa kwa Mola wa walimwengu. Napenda matendo yangu yapandishwe hali ya kuwa nimefunga.”

Kumethibiti Hadiyth kwa jumla zinazokokoteza juu ya kufunga siku tatu kwa kila mwezi, kufunga masiku meupe kila mwezi; siku hizo ni 13, 14 na 15, kufunga miezi mitukufu na kufunga Jumatatu na Alkhamisi. Rajab inaingia katika jumla hiyo. Ikiwa ni mtu mwenye pupa kuchagua kufunga mwezi maalum basi afunge masiku matatu meupe au siku ya Jumatatu na Alkhamisi. Vinginevyo mambo ni sahali.

Kuhusiana na kukhusisha siku maalum kufunga Rajab hatujui kuwa kitendo hicho kina asli katika Shari´ah.

  • Mhusika: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (02/363)
  • Imechapishwa: 24/08/2020