Kufunga siku maalum kwa ajili ya kumshukuru Allaah


Swali: Je, inajuzu kwa mtu kufunga kwa ajili ya kumshukuru Allaah wakati anapopata neema, kama kuruzukiwa mtoto au kupata khabari nzuri, akafunga siku moja au mbili kwa kumshukuru Allaah kwa hilo au atosheke na kusujudu Sujuud-ush-Shukr tu?

Jibu: Yote mawili. Muusa (´alayhis-Salaam) alifunga siku ya ´Aashuuraa kwa kumshukuru Allaah kuunusuru Uislamu. Hili pia ni katika kumshukuru Allaah. Swawm ni katika kumshukuru Allaah, Sujuud-ush-Shukr na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (38) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-01-06.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014