Swali 822: Inafaa kwa muumini kufunga ndoa na mke wake wa Ahl-ul-Kitaab kanisani na kupitia mkono ya padiri baada ya kufunga naye ndoa kwa mujibu wa Sunna ya Allaah na ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye ofisi za ndoa za kingereza?

Jibu: Haijuzu kwa muumini kufunga ndoa na mke wake – wa kiislamu au wa Ahl-ul-Kitaab – ndani ya kanisa wala kupitia mikono ya padiri. Hata kama hayo yatafanyika baada ya Sunnah ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu katika kufanya hivo kuna kujifananisha na manaswara katika nembo za ndoa zao, kukuza nembo zao, masinagogi, kuheshimu wasomi wao, ´ibaadah zao na kuwaheshimu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Ameipokea Imaam Ahmad kwa cheni ya wapokezi nzuri.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 324
  • Imechapishwa: 27/07/2019