Anataka kufunga masaa 24 na kuzingatia amefunga siku mbili

Swali: Je, mtu anaweza kufunga siku tatu usiku na mchana katika Ramadhaan na ni badala ya siku thelathini?

Jibu: Haijuzu kufanya hivo na hakuna mwanachuoni yeyote aliyesema hivo. Kwa sababu Kwa sababu usiku sio wakati kufunga. Mwenye kufanya hivo anazingatiwa ameenda kinyume na Shari´ah, amefanya kitu ambacho hakikuwekwa na Allaah katika Shari´ah na amefungua katika Ramadhaan bila ya udhuru. Jengine ni kwa sababu Allaah amewawajibishia wale ambao ´ibaadah ni zenye kuwawajibikia katika waislamu kufunga Ramadhaan yote. Kwa hiyo kufunga baadhi ya siku hazitoshelezi kutokamana na zengine.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (3089)
  • Imechapishwa: 24/04/2020