Swali: Sisi tuko na mwanamke anayeishi katika nchi ya kikafiri na wala havai Hijaab ili asifukuzwe kazini kwake. Anajengea hoja kwamba uchaji Allaah mahali pake ni moyoni…

Jibu: Mahali pake ni moyoni na huonekana katika viungo vya mwili. Uchaji Allaah huonekana kwenye viungo vya mwili kwa kutendea kazi Sunnah. Madai haya huyadai watu waovu na ni madai batili. Ni kweli kwamba kumcha Allaah kunakuwa moyoni, lakini huonekana kwenye viungo vya mwili na kwenye matendo. Kusema kwamba uchaji Allaah uko moyoni na unafanya utakavyo ni kitu kisichojuzu. Yeye ni muislamu na hivyo ni lazima kujisitiri. Ima wamkubalie au atafuta kazi nyingine. Riziki iko mikononi mwa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 22/04/2021