Kufuga ndevu ni faradhi na wajibu


Swali: Ni ipi hukumu ya kufuga ndevu?

Jibu: Ni faradhi na wajibu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ziacheni ndevu na punguzeni masharubu.”

Abu Muhammad bin Hazm amesema:

“Wanachuoni wamefikiana juu ya kwamba kuziacha ndevu ni faradhi na kwamba kuzinyoa ni haramu.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=67941&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 29/07/2017