Kufuatilia darsa kwa njia ya intaneti ni sawa na msikitini?


Swali: Je, kuhudhuria mihadhara kwa njia ya intaneti na kusikiliza mtu anapata ujira kama mfano wa ujira anaopata mtu kwa kuhudhuria misikitini kwa wanachuoni?

Jibu: Misikiti ina mambo yake maalum.

1) Kuna utulivu

2) Rehema.

3) Malaika.

4) Nyumba ya Allaah.

Kuhudhuria msikitini na kusikiliza darsa na mihadhara, bila ya shaka hili ni bora zaidi, sawa bila kujali sehemu yoyote ile.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13252
  • Imechapishwa: 20/09/2020