Kufikiria sana ndani ya swalah kunaiharibu swalah?

Swali: Swalah yangu ni yenye kubatilika ikiwa sehemu yangu kubwa ya Swalah ninafikiria mambo ya kidunia?

Jibu: Hapana, halibatilishi Swalah yako. Lakini linabatilisha thawabu zake. Anayefikiria katika Swalah yake, huyu hatorudi kuswali tena. Lakini hata hivyo hana thawabu isipokuwa kwa kiasi cha jinsi moyo wake ulivokuwa umehudhuria ndani yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-4-23.mp3
  • Imechapishwa: 09/11/2014


Takwimu
  • 25
  • 413
  • 1,821,444