Swali: Ikiwa ´iyd itaangukia siku ya alkhamisi lakini hilo halikujulikana isipokuwa baada ya jua kupinduka. Je, wale wataoswali swalah ya ´iyd siku ya kufuatia, nayo ni siku ya ijumaa, hawahitajii kuswali swalah ya ijumaa?

Jibu: Swalah ya ijumaa haianguki. Ni lazima iswaliwe. Lakini yule atakayeswali swalah ya ´iyd si lazima kwake kuhudhuria swalah ya ijumaa. Si lazima kwa mtu mmoja mmoja. Ama watu kwa jumla ni lazima waswali swalah ya ijumaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (14) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-03-11-1434.mp3
  • Imechapishwa: 01/06/2019