Kufanya yaliyoamrishwa au kuacha yaliyokatazwa?

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

09- Abu Hurayra ´Abdur Rahman bin Swakhr (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Kile nilichokukatazeni kiepukeni na kile nilichokuamrisheni fanyeni kwa wingi kadiri muwezavyo… “

Lipi bora zaidi; kuacha yaliyokatazwa au kufanya yaliyoamrishwa? Wanachuoni wametofautiana katika hili juu ya kauli mbili:

1- Mosi: Kuacha yaliyokatazwa ndio bora zaidi kuliko kufanya yaliyoamrishwa. Wametumia dalili ikiwa ni pamoja na Hadiyth hii ambapo ameamrisha kuepuka kabisa yale aliyokataza na hivyo wakawa wamesema kuepuka ndani yake kuna makalifisho kwa kuwa ni mambo yanayohusiana na mataamnio. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pepo imezungukwa na mambo yenye kuchukiza na Moto umezungukwa na mambo ya matamanio.” (al-Bukhaariy (6487))

Kwa hivyo wakawa wamesema mtu kujiepusha na yaliyokatazwa ndio bora zaidi.

2- Pili: Kundi lingine katika wanachuoni likasema kufanya yaliyoamrishwa ndio bora zaidi na ni jambo lenye ngazi ya juu. Wametumia dalili ikiwa ni pamoja na kwamba Aadam (´alayhis-Salaam) Malaika waliamrishwa kumsujudia. Ibliys akakataa kutekeleza amri hii na hivyo akawa amekhasirika duniani na Aakhirah. Akalaaniwa mpaka siku ya kufufuliwa na ataingizwa Motoni milele. Hili ni kutokana na ukubwa wa maamrisho. Vilevile wakasema tena ya kwamba Aadam alikula kwenye mti aliyokatazwa na baadaye akawa amesamehewa. Ibliys aliamrishwa amri ambayo hakuitekeleza na akawa amekhasirika. Vilevile na Aadam (´alayhis-Salaam) alifanya aliyokatazwa kisha baadaye akasamehewa kwa kuomba msamaha.

Kauli hii ya pili ndio yenye nguvu na ilio wazi. Kwa kuwa kufanya yaliyoamrishwa ndio jambo lenye daraja ya juu. Ama kufanya yaliyokatazwa ni jambo liko kwenye matarajio ya kusamehewa. Kuhusiana na mtu kupuuzia kufanya yaliyoamrishwa, kama kwa mfano kupuuzia kufanya mambo ya wajibu ya Kishari´ah na mambo ya faradhi, nguzo na mfano wa hayo, haya ni mambo yalio makubwa kuliko Aliyokataza Allaah (Jalla wa ´Alaa).

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 184-185
  • Imechapishwa: 17/05/2020