Kufanya utalii sehemu kama za kina Thamuud, ´Aad na Madyana

Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya zile sehemu za kina Thamuud kuwa ni mahali pa kutalii?

Jibu: Haijuzu kuingia sehemu kama hizo isipokuwa ikiwa kama mtu atalia. Kutokana na Hadiyth yenye kusema:

“Ikiwa hamkulia basi jilizeni.”

Haijuzu kuuingia isipokuwa kwa namna iliyotajwa katika Hadiyth:

“Msiingie nyumba za wale waliodhulumu isipokuwa ikiwa kama mtalia kwa kuchelea msije kupatwa na kilichowapata.”

Kwa ajili hii wakati  Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipopita sehemu hiyo aliinamisha kichwa chake na akaharakisha mwendo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 15/05/2019