Swali: Je, inajuzu kufanya Twawaaf katika wakati ambapo Khatwiyb anatoa Khutbah ya Ijumaa na kabla ya kukimu Swalah ya Ijumaa?
Jibu: Ndio, hakuna neno atukufu hata kama Imamu anatoa Khutbah ya Ijumaa. Atufu. Ikiwa atakaa na kusikiliza Khutbah na akachelewesha Twawaaf [baadae], ndio bora. Lakini lau atatufu Twawaaf yake ni sahihi. Hata kama lau atatufu na kunaswaliwa Tarawiyh au kunatolewa Khutbah, hakuna neno.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (21) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-04-06.mp3
- Imechapishwa: 14/11/2014