Kufanya Twawaaf baada ya hedhi kusita kwa masaa kadhaa


Swali: Mwaka huu nilihiji na katikati ya Twawaaf-ul-Ifaadhwah nikatokwa na damu. Nikamweleza daktari jambo hilo ambapo akanieleza kuwa atanipa vidonge vitavyozuia damu kwa muda wa masaa sita. Mambo yakawa kama alivyosema damu ikasita kwa muda wa masaa sita ambapo niafanya Twawaaf na Say´  na baada ya masaa sita damu ikarudi. Je, niliyoyafanya ni sahihi?

Jibu: Ikiwa kusita kwa damu ililkuwa twahara kamilifu na mwanamke huyo anajua kutwaharika basi hakuna neno. Twawaaf yake itakuwa ni sahihi. Ama kama ilikuwa sio twahara sahihi, basi ametufu kabla hajatwaharika. Twawaaf ya mwanamke kabla ya kutwaharika kwake ni batili na si sahihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (65) http://binothaimeen.net/content/1467
  • Imechapishwa: 14/01/2020