Kufanya Tayammum na kuswali kwa wakati au mtu atafute maji?

Swali: Nikiwa sina maji na nikachelea jua lisichomoza na wakati wa swalah ukaisha – je, mtu ayatafute maji pamoja na kwamba wakati utaisha au afanye Tayammum?

Jibu: Afanye Tayammum. Lakini wanachuoni wamesema kuwa Tayammum inakuwa mwishoni mwa wakati. Kuswali kwa kutawadha kwa maji ndio bora zaidi ikiwa mtu ana matarajio ya kuyapata maji. Katika hali hii bora ni mtu kuchelewesha swalah mpaka wakati wake wa mwisho. Ama akichelea wakati kutoka basi ni wajibu kwake kufanya Tayammum na asiache wakati ukaisha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 22/02/2019