Swali: Ipi hukumu ya “al-Arba´iyniyyah” yaani mwanamke mwenye nifasi damu yake inapokatika na akatwahirika damu yake huita kuwa ni “al-Arba´iyniyyah” halafu wakafanya sherehe, wanakusanyika wanawake wengi na kusherehekea kwa kula na kunywa n.k?

Jibu: Hili sikunasihi, nakunasihi kuliacha. Si katika mfumo wa Salaf. Hili ni jambo la kwanza.

Jambo la pili ni kuwa mpaka wa kuifanya nifasi hukatika siku arubaini, huu ni wingi tu wa nifasi. Mwanamke anaweza kutwahirika kabla ya siku hizo. Wasidhani baadhi ya wanawake kuwa nifasi yake haikatiki ila mpaka zitimie siku arubaini, asidhanie hivyo. Akaacha kufanya ´ibaadah akawa haswali, hafungi akamnyima mke wake haki yake akidhani mpaka zitimie siku arubaini.

Jambo la tatu hakuna haja ya kutangazia kuwa umetwaharika. Unaweza kutwaharika mnamo siku ishirini, kumi au siku thelathini, hakuna mpaka. Hii ni siri baina yake yeye na mke wake, hata wakaazi wa nyumbani kwake, haifai wao kujua (kuwa ametwaharika). Hili ni jambo baina yake yeye na mume wake. Labda tu wajue kwa njia ingine – wakuone kwa mfano umeanza kuswali tena. Nakunasihi kuacha jambo hili, na Uislamu ni [dini] inapenda kusitiri. Na nyinyi hali kadhalika mnatakiwa kupenda akipendacho Allaah na Mtume Wake – kusitiri.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=2407
  • Imechapishwa: 24/09/2020