Swali: Unasemaje juu ya kucheza na kaptula na ikaonekana sehemu ya mapaja?

Jibu: Haijuzu kucheza na kaptula. Wanachuoni wamevutana juu ya mapaja kama ni kiungo kisichotakiwa kuonekana (´Awrah) au sivyo. Maoni ya sawa ni kwamba ni kiungo kisichotakiwa kuonekana. Kumepokelewa Hdiyth kadhaa zinazojulisha kuwa ni kiungo kisichotakiwa kuonekana. Isitoshe ni njia inayopelekea kufunua viungo vikubwa visivyotakiwa kuonekana. Kwa hivyo maoni ya sawa ni kwamba mapaja ni kiungo kisichotakiwa kuonekana na kwamba haifai kucheza kwa kaptula. Ni mamoja mpira wa miguu au mchezo mwingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4062/حكم-لعب-الرياضة-بسراويل-تكشف-الفخذ
  • Imechapishwa: 01/11/2020