Kufanya kazi benki kwa sababu ya haja

Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya kazi benki kutokana na haja?

Jibu: Haijuzu kufanya kazi benki. Benki zina miamala ya ribaa na hivyo hiajuzu kufanya kazi ndani yake. Kwa sababu huko ni kusaidiana katika dhambi na uadui. Haijuzu kusaidiana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mla ribaa, mwakilishi wake, mwandishi wake na shahidi wake. Amesema:

“Wote wanalingana.”

Mwandishi na mwenye kushuhudia ribaa ni wenye kushiriki. Anayewateua anakuwa ima ni mhasibu, mwagizaji au msimamizi. Ndani yake kuna kuwasaidia juu ya mabalaa yao.

Swali: Vipi kuhusu yule ambaye anahifadhi pesa yake humo?

Jibu: Haitakikani kuzihifadhi humo. Lakini hakuna neno endapo haja itapelekea yeye kufanya hivo. Dharurah ni kama yeye kuzihifadhi humo kwa sababu ya kuchelea pesa zake na wakati huohuo hana mahali pengine anaweza kuzihifadhi. Hivyo azihifadhi humo bila ya kupokea faida.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4290/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D9%85%D9%84-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D8%A8%D9%86%D9%88%D9%83-%D9%84%D9%84%D8%AD%D8%A7%D8%AC%D8%A9-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%B6%D8%B1%D9%88%D8%B1%D8%A9
  • Imechapishwa: 02/07/2020