Kufanya jimaa kwa kondomu bila kumwaga


Swali: Kuna mwanaume alitumia kondomu wakati wa kufanya jimaa na mke wake. Hakumwaga manii. Je, ni lazima aoge?

Jibu: Ni wajibu kwake kuoga. Hata hivyo kuna wanachuoni wanaosema kuwa sio wajibu kuoga kwa sababu tupu mbili hazikukutana.

Swali: Lakini lililo salama zaidi ni yeye kuoga?

Jibu: Ndio, ndili salama zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (18 B) http://audio2.islamweb.net/lecturs/mal3othemen/bab/18/18.mp3
  • Imechapishwa: 17/09/2017