Swali: Hakika Bid´ah zinakuwa nyingi katika mwezi wa Rajab. Je, una chochote cha kuwaambia wale wanaoelezea Bid´ah na ´ibaadah mbalimbali katika mwezi huu?

Jibu: Mwezi wa Rajab hauna Sunnah. Lakini hata hivyo hakuna ubaya kufanya ´Umrah  ndani yake. as-Salaf as-Swaalih walikuwa wakifanya ´Umrah katika Rajab. Vilevile imethibiti kutoka kwa Ibn ´Umar aliyesema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya ´Umrah katika Rajab. Kwa hivyo kufanya ´Umrah katika Rajab ni sawa.

Ama kuufanya ni mwezi maalum kwa ajili ya ´ibaadah ni jambo halina msingi. Ni mwezi kama mingine. Mtu anaweza kuswali, kufunga masiku tatu kila mwezi, kufunga jumatatu na alkhamisi kama miezi mingine. Mtu asifanye chochote maalum ndani yake mbali na ´Umrah. Katika hali hiyo hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb http://www.alifta.net/Fatawa/FatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=342&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 22/03/2018