Kufanya biashara baada ya adhaana

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anauza baina ya adhaana na Iqaamah mbele ya milango ya misikiti na kwenye njia? Je, akatazwe?

Jibu: Ndio, akatazwe. Kwa sababu kitendo hicho kinamshughulisha kutokamana na swalah. Aidha kitendo hicho kinaweza kumpelekea swalah kumpita au kupitwa na Takbiyrat-ul-Ihraam.

Kwa hivyo mwenye kukaa baada ya adhaana anatakiwa kuambiwa aswali. Lakini endapo atauza mauzo yake ni sahihi. Mwenye kufanya hivo si sawa na ambaye anauza baada ya wito wa ijumaa. Mauzo baada ya wito wa ijumaa hayajuzu. Ama mauzo baada ya wito wa vipindi vitano mauzo hayajuzu. Lakini hata hivyo anatakiwa kuamrishwa kuswali na kuacha kufanya mauzo ili kusimshughulishe kutokamana na kuswali.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (12) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191546
  • Imechapishwa: 31/08/2019