Kufaa kuswali kazini kunapokhofiwa madhara

Swali: Sisi ni takriban wafanyakazi kumi ambao tunafanyakazi katika benki ya Kiislamu. Swalah ya Maghrib inatufikia ilihali bado tuko kazini. Je, inajuzu kwetu kuswali kazini pamoja na kuzingatia ya kwamba msikiti uko karibu nasi. Ni kwa vile wakati wa kumaliza kazi tunakuwa na mambo mengi jambo ambalo linapelekea tunakosa swalah ya mkusanyiko. Tufanye nini?

Jibu: Ikiwa kutoka kwenu hapo benki na kwenda msikitini kunaathiri madhara au kunakhofiwa wezi na mfano wa hayo, hakuna neno mkabaki na mkaswali mahali mlipo.

Swali kama mlivosikia ´benki ya Kiislamu`. Kwa msemo mwingine ni kwamba haina ribaa kabisa. Huu ni udhuru. Kiasi cha kwamba wanachuoni wamesema kwamba mwokaji akichelea endapo ataenda msikitini basi mikate itachomeka, basi inafaa kwake kubaki. Mikate si kitu ukilinganisha na pesa. Isitoshe wanachuoni wamesema kuwa huyo mwokaji amepewa udhuru wa kuacha swalah ya mkusanyiko pamoja na kuwa watu hawa wataswali swalah ya mkusanyiko. Sioni kama kuna ubaya kwao ikiwa kwenda kwao msikitini kutapelekea katika madhara au kunakhofiwa wezi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (60) http://binothaimeen.net/content/1362
  • Imechapishwa: 25/11/2019