Kufa na imani kwamba Allaah yuko kila mahali


ali: Mwenye kufa juu ya ´Aqiydah ya kwamba Allaah Yuko kila mahali na anahifadhi swalah na nguzo zingine. Je, mtu aseme kuwa ni katika watu wa Peponi au wa Motoni?

Jibu: Jambo lake liko kwa Allaah. Mara nyingi anakuwa na kupindisha maana na kufuata kichwa mchunga huku akidhani kuwa ni sahihi. Ama ikiwa ni mwenye kukusudia, huyu ni kafiri. Lakini inawezekana kuwa hakukusudia na anafikiria waliokuwa kabla yake na waliomtangulia wako katika haki na ni wanachuoni, kadhalika wameziwekea upindishaji wa maana Aayah na akafikiria kuwa hili ni sahihi. Allaah ndiye Anajua zaidi. Hili tunamwachia Allaah (´Azza wa Jalla).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (63) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13810
  • Imechapishwa: 16/11/2014