Kuenea kwa maasi katika jamii ni udhaifu wa Tawhiyd

Swali: Kuenea kwa maovu kunazingatiwa ni kudhoofika kwa Tawhiyd kati ya watu?

Jibu: Ndio, ni kudhoofika kwa imani mtu kujitanguliza kwenye maasi. Mtu akiwa na imani yenye nguvu anajitenga mbali na maasi. Hakuna anayeyaendea maasi isipokuwa yule mwenye imani dhaifu, uchache wa elimu na kumwogopa Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 94
  • Imechapishwa: 25/07/2019