Kuendesha gari kwa kasi ili kuwahi swalah ya mkusanyiko

Swali: Ni ipi hukumu ya kuendesha gari kwa kasi wakati wa kuharakia swalah ya mkusanyiko?

Jibu: Haijuzu kuendesha gari kwa kasi kwa wala kwa miguu. Kuna khatari kwenda kasi kwa gari. Haijuzu kwa mtu kuiweka khatarini nafsi yake. Haifai kwake kuvunja alama za barabarani wala kuzivuka[1]. Kufanya hivo kuna khatari.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kikomo-cha-kasi-kinatakiwa-kufuatwa/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 18/09/2021