Kudumu kwa kusoma Qur-aan na kufanya Adhkaar ni kinga ya muislamu

Swali: Kudumu kwa kusoma Qur-aan ni miongoni mwa tiba za uchawi?

Jibu: Unajilinda dhidi ya uchawi. Kudumu kwa kusoma Qur-aan, kufanya Adhkaar na nyuradi zilizowekwa katika Shari´ah ni kinga. Ni mambo yanamkinga mtu na uchawi, kijicho, hasadi, mashaytwaan wa kijini na wa kiwatu na mengineyo. Ni ulinzi. Kumdhukuru Allaah ni kinga ya muislamu anayojikinga nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (07) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/07.mp3
  • Imechapishwa: 12/01/2019