Kudhihirisha maovu ya mtawala mbele za watu

Swali: Inafaa kudhihirisha kasoro za mtawala wa waislamu mbele ya jamii na mbele za watu?

Jibu: Mmekwishasikia jawabu mara nyingi tu ya kwamba haijuzu kuwasema vibaya watawala. Hili linasababisha shari, jamii kumwaga damu, kufarikisha umoja wa waislamu, wananchi kumchukia mtawala mpasuko na shari. Jambo linaweza kupelekea watu wakamfanyia uasi mtawala, kumwagika damu na mambo ambayo mwisho wake ukawa mbaya. Ukiwa na jambo basi mfikishie mtawala kwa njia ya siri. Ima unaweza kumfikishia kwa kumwambia kwa mdomo ukiweza kufanya hivo au kwa kumwandikia barua na kuwapigia simu na kuwafikishia. Kumpa nasaha mtawala inakuwa kwa njia ya siri. Haiwi hadharani. Haya yamekuja katika Hadiyth:

“Yule anayetaka kumnasihi mtawala basi amshike mkono na amnasihi kwa siri.”

Kumekuja maana kama hii katika Hadiyth.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidhl-il-Islaam (08) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/08.mp3
  • Imechapishwa: 16/02/2019