Kuchukua picha sehemu ya uso


Swali: Ni ipi hukumu ya kumchukua picha mtu na khaswa upande wa uso wake?

Jibu: Kichwa kikiondoshwa kutoka kwenye picha yameondoka makatazo. Picha ikiwa haina kichwa hakuna neno. Kwa msemo mwingine kichwa kikaondoshwa chote na sio uso peke yake. Kichwa kikiondoshwa yameondoka makatazo. Kichwa kikikatwa na kuondoshwa yameondoka makatazo. Kupiga msitari haitoshi; ni lazima kichwa chote kiondoshwe. Kichwa chote kiondoshwe ili mwili ubaki ukiwa hauna kichwa. Katika hali hiyo yameondoka makatazo na wala haizuii Malaika kuingia.

 

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=4xTg13fHGuU
  • Imechapishwa: 19/11/2017