Kuchukua elimu ya Fiqh kwa Suufiyyah


Swali: Inajuzu kuchukua elimu ya Fiqh kwa Suufiyyah na wanachuoni wa Suufiyyah?

Jibu: Allaah amekutosheleza nao. Wanachuoni wa Sunnah ni wengi na himidi zote ni Zake Allaah. Tafuta elimu kwa wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah hata kama hili litahitajia kusafiri na kuwaendea. Na si lazima ukae miaka, hata kama itakuwa kwa mwezi mmoja au nusu ya mwezi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Imechapishwa: 04/09/2020