Swali: Je, inajuzu kwa mtu ambaye hamiliki thamani ya Udhhiyah kwa hivi sasa kukopa ili aweze kununua mnyama wa Udhhiyah kisha atamlipa rafiki yake deni hili huko baadaye? Mtu huyu yuko na miti inayozalisha matunda ambayo anachuma kutoka hapo.

Jibu: Ndio, imependekezwa kwake. Imependekezwa kwake kuchukua deni na akachinja ikiwa nyuma yake ameacha kitu cha kumtosheleza. Ikiwa nyuma yake ameacha cha kumtosheleza basi imependekezwa kwake kuchinja Udhhiyah ijapokuwa itakuwa ni kwa kuchukua deni. Ikiwa huko baadaye anaweza kulipa deni hilo na yuko na cha kumtosheleza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/10823/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B3%D8%AA%D8%AF%D8%A7%D9%86%D8%A9-%D9%84%D8%A7%D8%AC%D9%84-%D8%B4%D8%B1%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B6%D8%AD%D9%8A%D8%A9
  • Imechapishwa: 16/08/2018