Swali: Je, ni sahihi kuchinja wanyama wawili; mmoja kwa ajili ya Udhhiyah na mwingine kwa ajili ya kugawa nyama yake? Ni ipi hukumu ya mnyama wa Udhhiyah ambaye amekatika sikio au pembe?

Jibu: Hili ni swali zuri. Sunnah ni yeye kuchinja kichinjwa kimoja kwa ajili yake yeye na watu wa nyumbani kwake. Hivyo ndivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivokuwa akifanya. Sisi tunatambua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye kiumbe mkarimu zaidi wa watu. Lakini hata hivyo alichinja kichinjwa kimoja tu. Kutekeleza Sunnah ndio bora zaidi. Lakini akiongeza kichinjwa kingine kwa sababu aliyotaja hakuna neno – Allaah akitaka.

Kuhusu mnyama ambaye sikio na pembe lake limekatika maoni sahihi ni kwamba anasihi. Lakini hata hivyo amechukizwa. Kwa sababu ni mpungufu wa maumbile. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kutukuza jicho na sikio. Bi maana kutafuta utukufu na ukamilifu wavyo[1].

[1] Ahmad (01/149), at-Tirmidhiy (1948), an-Nasaa´iy (4462), Ibn Maajah (3142) na (3143).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (25/39)
  • Imechapishwa: 20/08/2018