Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anamchinjia Udhhiyah nduguye aliyekwishakufa?

Jibu: Hakuna neno. Ni swadaqah miongoni mwa swadaqah. Ikiwa ni wasia basi ni lazima kuutekeleza. Isipokuwa wasia basi washiriki. Waliohai na waliokwishakufa wanatakiwa kushiriki katika kichinjwa kimoja. Kilichotangaa kwa Fuqahaa´ ni kwamba inafaa kumchinjia maiti na kwamba ni swadaqah miongoni mwa swadaqah. Baadhi ya wanachuoni wameonelea kwamba ni jambo ambalo halikusuniwa na kwamba ni jambo limesuniwa kwa waliohai pasi na wafu. Lakini hata hivyo akimchinjia ambaye kishakufa thawabu zitamfikia ingawa haikusuniwa kwake kumchinjia kichinjwa maalum. Kwa hivyo akimshirikisha katika Udhhiyah yake hakuna neno.

Baadhi ya watu wasiokuwa na elimu wanawafanyia Udhhiyah wafu wao na hawajifanyii wao wenyewe wala waliohai. Udhhiyah ni kitu kilichosuniwa kwa ambaye yuhai kabla ya mtu. Kwa hivyo akijifanyia Udhhiyah yeye mwenyewe, watu wa nyumbani kwake kisha akawashirikisha wafu hakuna neno. Na ikiwa ni wasia unatakiwa kutekelezwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
  • Imechapishwa: 02/01/2021