Kuchinja Udhhiyah katika nchi za kimasikini Afrika, Asia na kwenginepo

Swali: Muislamu anaishi katika nchi isiyokuwa ya Kiislamu. Akichinja Udhhiyah basi huenda asimpate mwenye kuhitaji ambaye anaweza kumlisha. Yeye anaona kuagiza thamani yake kuwatumia mafukara wa Kiislamu au ichinjwe nchini mwao. Unasemaje juu ya hili?

Jibu: Hakuna neno kufanya hivo akamtuma [mnyama] huko kwengine. Hili ni jambo zuri. Inatakiwa iwe kupitia mikononi mwa watu waaminifu. Vilevile akituma thamani yake hakuna neno. Lakini ikiwa ni jambo lenye kuwezekana kumchinja pale anapoishi ili marafiki zake na ndugu zake waweze kumla ndio bora zaidi. Aitekeleze Sunnah mahali pake sehemu ambayo kuna waislamu wachache na akawapa ndugu zake wahitaji na waislamu. Vilevile hakuna ubaya akawapa mpaka makafiri midhali si wale makafiri wenye kuupiga vita Uislamu. Tunamaanisha wale makafiri wa amani ambao hawaupigi vita Uislamu. Kwa sababu hii ni swadaqah ya kujitolea. Pia akimtuma kwa mafukara huko Afrika, kwa wapambanaji huko Afghanistan au akatuma thamani yake yote ni sawa ikiwa hapo anapoishi hakuna ambao wanaweza kumla na wakafaidika na mnyama huo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11395/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B0%D8%A8%D8%AD-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B6%D8%AD%D9%8A%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D8%BA%D9%8A%D8%B1-%D9%85%D9%83%D8%A7%D9%86-%D8%A7%D9%82%D8%A7%D9%85%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B6%D8%AD%D9%8A-%D8%A7%D9%88-%D8%A7%D8%B1%D8%B3%D8%A7%D9%84-%D8%A8%D9%82%D9%8A%D9%85%D8%AA%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 16/08/2018