Swali: Katika mji wetu kumekuwa na ada katika misimu mbalimbali kama kuchinja tarehe 15 Sha´baan, mwanzoni mwa Ramadhaan na tarehe 27 Rajab. Je, inajuzu kula katika vichinjwa kama hivi?

Jibu: Kuhusu kuchinja tarehe 15 Sha´baan au tarehe 27 Rajab ni Bid´ah isiyokuwa na msingi. Haijuzu kufanya hivo wala kula katika kichinjwa hicho kwa kukosekana dalili. Bali hiyo ni Bid´ah.

Lakini kule kujikurubisha katika Ramadhaan kwa kuchinja na kutoa swadaqah, basi itambulike kuwa Ramadhaan ni mwezi uliobarikiwa na imewekwa katika Shari´ah kutoa swadaqah na kuwapa matumizi mafukara. Kwa hivo akichinja katika Ramadhaan, mwezi wa Dhul-Hijjah au wakati mwingine wowote na akaitoa swadaqah yote haya ni mazuri. Ama kufanya jambo ni maalum kwa ajili ya nusu ya Sha´baan au tarehe 27 Rajab – kama wanavyofanya baadhi ya watu ambapo wanasherehekea katika usiku huu – ni mambo yasiyokuwa na msingi. Bali ni Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb http://www.alifta.net/Fatawa/FatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=351&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 22/03/2018