Swali: Je, Udhhiyah ni wajibu? Mtu akiwa ni muweza na asichinje na hivi sasa umri wake ni karibu miaka arubaini pamoja na kuwa ana pesa nyingi sasa.

Jibu: Udhhiyah ni Sunnah iliyokokotezwa kwa mujibu wa wanachuoni wengi na sio wajibu. Abu Haniyfah ndiye anaonelea kuwa ni wajibu. Lakini wanachuoni wengi wanaonelea kuwa ni Sunnah iliyosisitizwa. Ni ´ibaadah ilio kubwa katika masiku ya ´Iyd. Kwa hivyo ni ´ibaadah ilio kubwa ambayo haitakiwi kwa muislamu kuiacha ikiwa ni muweza. Mtu anaweza hata kuchukua deni. Ikiwa mtu anaweza kulipa na akawa amechukua deni ili aweze kuchinja ni jambo zuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaa al-Hawaa´ http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1436-03-02.mp3
  • Imechapishwa: 01/12/2017