Kuchinja kwenye kaburi shirki kubwa au ndogo?

Swali: Mtu akichinja Udhhiyah yake kwenye kaburi fulani kwa kutaraji baraka ziteremke juu ya kichinjwa chake. Je, kichinja hichi kinazingatiwa kuwa ni shirki kubwa au shirki ndogo?

Jibu: Ikiwa amemchinjia maiti au amelichinjia kaburi ni shirki kubwa. Ama ikiwa amechinja kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall), lakini anadhani kuwa mahali hapa kuna fadhilah, basi hii ni shirki ndogo na ni njia inayopelekea katika shirki kubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 57