Swali: Ni ipi hukumu ya kuchinja kwa mkono wa kushoto?

Jibu: Kuchinja ni kitendo cha ´ibaadah na ni kitendo kitukufu. Msingi wa kutumia mkono wa kuume na mkono wa kushoto ni kwamba mkono wa kuume unatumiwa juu ya vitu vitukufu na mkono wa kushoto unatumiwa juu ya vitu vichafu. Kwa hivyo bora na Sunnah ni yeye achinje kwa mkono wake wa kulia. Akichinja kwa mkono wa kushoto inasihi na atakuwa ameacha lililo bora.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://saleh.af.org.sa/sites/default/files/2018-01/09.mp3
  • Imechapishwa: 07/09/2022