Kuchinja kichinjwa katika Sha´baan


Swali: Mimi nimezowea tangu nilipokuwa mdogo kuchinja kichinjwa au kwa msemo mwingine kutoa swadaqah katika mwezi wa Sha´baan katika usiku wowote wa mwezi huu. Je, kuna kitu juu yangu kwa kufanya hivo?

Jibu: Kutoa swadaqah – na khaswa zile swadaqah zenye kuendelea – ni miongoni mwa aina kubwa ya ´ibaadah. Lakini pamoja na hivyo kwa sharti iwe imeafikiana na Shari´ah takasifu, iwe imetokamana na chumo la halali na iwe imetolewa kwa njia inayokubalika katika Shari´ah. Kwa mfano kuwapa swadaqah mafukara na masikini, kujenga misikiti na mengineyo.

Haifai kutoa swadaqah katika wakati fulani kwa njia maalum ambayo haikuanishwa na Shari´ah na kuegemeza imani fulani. Ikiwa kitendo hichi amekifanya katika mwezi wa Sha´baan kwa kuamini imani fulani katika mwezi huu au katika siku yoyote basi si katika ´ibaadah zinazokubaliwa na Shari´ah.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alifta.net/Fatawa/fatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=4&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 18/04/2018