Kuchezesha simu wakati wa Khutbah


Swali: Je, inajuzu kucheza na simu katikati ya Khutbah ya ijumaa?

Jibu: Hapana. Haijuzu kucheza na kitu; sawa ikiwa ni simu, Siwaak, kalamu au kitu kingine chochote. Haijuzu kucheza na huku imamu yuko anatoa Khutbah. Ni wajibu kukaa kimya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fth-mjd-01061435-01.mp3
  • Imechapishwa: 19/09/2020