Kuchelewesha swalah mwanzoni mwa wakati wake mpaka mwishoni mwake

Swali: Wakati mwingine hatumalizi mihadhara isipokuwa saa 12.30 au 12.40 wakati ambapo swalah ya Dhuhr inaingia 11.30. Je, tunapata dhambi kwa kuchelewesha?

Jibu: Kuswali mwanzoni mwa wakati ndio bora zaidi. Lakini ukichelewesha kwa sababu zinazojitokeza katikati ya wakati hakuna neno. Kilicho haramu ni kuchelewesha mpaka ukatoka nje wakati wake. Ama midhali umechelewesha tu mwazoni mwa ule wakati wake ni jambo halina neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziy bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb http://www.alifta.net/Fatawa/fatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=1238&PageNo=1&BookID=5
  • Imechapishwa: 15/03/2018