Kuchelewesha sunnah ya ´ishaa mpaka wakati wa kulala

Swali: Je, inajuzu kuchelewesha Sunnah ya Raatibah ya swalah ya ´ishaa mpaka wakati wa kabla ya kulala?

Jibu: Maadamu bado imo ndani ya wakati, haina neno. Lakini hata hivyo bora zaidi ni kuharakisha kuifanya ili asiisahau au akasikia uvivu kuiswali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (68) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-05-21.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020