Kuchelewesha Maghrib mpaka wakati wa ´Ishaa

Swali: Mimi na familia yangu huenda mji mwingine ambao uko umbali wa 50 km kutoka mji wetu kwa ajili ya kununua baadhi ya mahitaji na tunarudi wakati wa Maghrib. Wakati mwingine tunarudi tumechelewa kwa sababu ya msongamano na ufinyo wa wakati wa Maghrib. Pengine tusifike isipokuwa pamoja na adhaana ya ´Ishaa baada ya kumalizika wakati wa Maghrib. Je, katika hali hii inafaa kwetu kutokana na umbali wa miji na ugumu unaowapata kina mama kuchelewesha Maghrib mpaka tufike katika mji wetu?

Jibu: Kutokana na hali iliyotajwa hapana neno kuchelewesha Maghrib mpaka utakapofika katika mji kwa ajili ya kuepuka ugumu. Ikiwepesika kuiswali njiani ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/386)
  • Imechapishwa: 02/10/2021