Kuchelewesha au kukusanya swalah kwa ajili ya kazi au masomo II

Swali: Tunajua kuwa kuchelewesha swalah kwa wakati wake ni dhambi. Lakini wakati mwingine kunatolea hali ambazo zinaweza kupelekea mtu kuchelewesha swalah kwa wakati wake. Kama kwa mfano mtu ni mchungaji wa kondoo na huku anasikia anadhaana inatolewa. Lakini hata hivyo nachelea kondoo wasije kuharibu vipandwa vya vyetu au vya jiarani yetu. Matokeo yake swalah ikanipita hata kama nitakuwa peke yangu au ukanipita wakati wa Dhuhr kama inavyotokea mtu yuko katika muhadhara au kazini. Ni zipi nasaha zenu?

Jibu: Ni wajibu kwa muumini atilie umuhimu swalah kwa wakati wake. Akiwa yuko katika mashamba ambayo anakhofia juu yake, basi atangulie kwanza kuwaweka wanyama hao mbali na mashamba kabla ya wakati haujaingia ili aweze kuswali kwa wakati wake au kuswali kwa mkusanyiko ikiwa yuko pambizoni na mkusanyiko au msikiti. Mtu asichukulie wepesi kunako jambo la swalah mpaka wakati ukawa mfinyu. Ni wajibu kwa mtu huyo kumcha Allaah na afanye sababu za kuhifadhi swalah kabla wakati wake [haujatoka] ili asitumbukie katika kujifananisha na wanafiki ambao wanaziharibu swalah:

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ

“Hakika wanafiki  wanafikiri wanamhadaa Allaah na [uhalisia wa mambo] Yeye ndiye anawahadaa na wanaposimama kuswali, basi husimama kwa uvivu.” (04:142)

Ni wajibu kwa waumini kutilia umuhimu jambo hili. Akiwa katika muhadhara au masomo basi asimamishe muhadhara au masomo na asimamishe swalah na aswali pamoja na waislamu katika misikiti yao. Ama akiwa sehemu ambazo si pambizoni na misikiti, bali ni mahali ambapo kunafanywa mihadhara au nad-wah, halafu baada ya hapo wanaswali kwa pamoja papo hapo, kama sehemu ambayo ni mbali na msikiti na karibu yake hakuna msikiti au jangwani au safarini, hali zote hizi hakuna neno. Wakimaliza basi wanachotakiwa ni kuswali kwa wakati na wasicheleweshe nje ya wakati wake. Bali wanachotakiwa ni kuswali kwa wakati wake.

Lakini yule ambaye yuko karibu na msikiti na yuko kijijini au mjini mwake, basi haifai kwake kuchelewesha swalah kwa sababu ya muhadhara, nad-wah, kondoo, ngamia au sababu nyenginezo. Ni wajibu kwake kutilia umuhimu yale yatayomsaidia kutekeleza swalah kwa mkusanyiko hata kama itahitajia kuwaweka kondoo au ngamia hao mbali na mashamba kabla ya kuingia wakati wake ili aweze kuswali swalah kwa wakati wake pamoja na waislamu wenzie. Haifai kwake kuchukulia wepesi jambo hili. Anapata dhambi kwa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziy bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb http://www.alifta.net/Fatawa/fatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=1239&PageNo=1&BookID=5
  • Imechapishwa: 15/03/2018