Kuchapuka kwa ajili ya kuwahi Rak´ah

Swali: Ni ipi hukumu ya kutembea haraka kuiwahi swalah?

Jibu: Mtu kufanya haraka wakati wa kutembea kuiwahi swalah ni jambo limekatazwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametuamrisha kutembea kwa utulivu na utaratibu na akatukataza kwenda matiti. Isipokuwa baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa hakuna ubaya kwenda haraka isiyokuwa mbaya pale ambapo mtu atachelea kupitwa na haraka. Kwa mfano mtu ameingia akamkuta imamu yuko katika Rukuu´ na hivyo akachapuka uchapukaji usiyokuwa mbaya kama unaofanywa na baadhi ya watu utawaona wanakimbia mbio sana, jambo ambalo limekatazwa. Pamoja na kwamba kuja kwa mwendo wa utulivu na utaratibu na kutofanya haraka ndio bora hata kama mtu atachelea kupitwa na Rak´ah. Hayo ni kutokana na ueneaji wa Hadiyth.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 307
  • Imechapishwa: 05/05/2020