Kuchanganyikana na watu au kujitenga?


Swali: Leo kujitenga na watu ndio bora zaidi kuliko kuchanganyika na watu kutokamana na kuwepo kwa fitina nyingi?

Jibu: Inategemea. Ikiwa anachanganyika na watu kwa ajili ya kuwalingania katika dini ya Allaah, kuwaamrisha mema na kukataza maovu, kuwanufaisha na kuwafunza watu, lililo bora zaidi ni kuchanganyika nao. Ikiwa hana haya yaliyotajwa hapa juu au hawezi, basi kujitenga kwake na watu ni bora zaidi. Kwa sababu kuchanganyika kunamdhuru zaidi na hakumnufaishi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsirayat-12-07-1435-01_0.mp3
  • Imechapishwa: 20/05/2018