Swali: Mimi nimfanya kazi ambaye nafanya kazi pamoja na kundi la waislamu katika kazi fulani. Lakini sijawahi kuwaona wafanya kazi hawa kumsujudia Allaah Rak´ah hata moja mbali na swalah ya ´Iyd mbili pekee kwa muda wa mwaka. Ni lipi la wajibu kwangu juu yao? Nimekwishawanasihi sana? Ni lipi la wajibu kwa mmiliki wa kazi? Unashauri nini? Je, kwa kuendelea kwao juu ya kitendo hicho wanakuwa makafiri kwa njia ya kwamba ni haramu kwangu kuanza kuwatolea salamu na kuwazungumzisha?

Jibu: Lililo la wajibu kwa yule ambaye anashirikiana na watu hawa katika kazi ilihali hawaswali aanze kwanza kuwanasihi, awatahadharishe kutokamana na adhabu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na awabashirie yale wanayopata pindi wataposimama kumtii Allaah. Yakiwanufaisha hayo basi ni vizuri. Yasipowanufaisha basi ni lazima kwake kumfikishia bosi wao wanayemfanyia kazi kuhusu hali zao. Huyu bosi ambaye wanamfanyia kazi ni lazima kwake kuwaamrisha kuswali. Wasipofanya hivo basi ni lazima kwake awasafirishe [kurudi kwao] kwani watakuwa hawana kheri yoyote. Haifai kuwanyamazia. Bali ni lazima aanze kuwanasihi kwanza. Ikishindikana awasafirishe kwenda katika nchi yao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (67) http://binothaimeen.net/content/1523
  • Imechapishwa: 14/02/2020