Kucha na nywele zinafanywa nini baada ya kukatwa?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuzika kucha na nywele baada ya kuzikata?

Jibu: Wanachuoni wamesema kuwa kuzika nywele na kucha ndio vizuri na bora zaidi. Hayo yamepokelewa kutoka kwa baadhi ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Si sawa kuyaacha sehemu ya wazi au kuyatupa katika mahali kunakopelekea katika dhambi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/132)
  • Imechapishwa: 30/06/2017